Categories: Voice of Reason

MJUMBE WA KAUNTI HAHITAJI SHAHADA – JOHN MRUTTU

By Eng John Mruttu

Wiki jana nikiwa Werugha katika eneo bunge la Wundanyi niliongelea Swala la Shahada kwa wagombea wa nafasi ya Mjumbe wa bunge la county yaani MCAs.

Nilikutana na watu kadha wa kadha ambao waliniuliza maoni yangu kuhusu swala hilo.

SOMA:  IS KENYA DERAILING INTO AN OLIGARCHY?

Mimi sioni kama ni sawa kulazimishia shahada ya chuo kikuu kwa wagombea nafasi ya MCAs.

Sababu zangu ni mbili

Ya kwanza ni kwamba watu wenye shahada za chuo kikuu ni wachache mno hapa nchini. Inakisiwa kwamba wako kama asilia moja. Na kuna watu wengine ambao hawana shahada kwa sababu Taifa letu halija jenga Vyuo Vikuu vya kutosholeza watu wote. Sasa kwa nini tuadhibu watu wengine kwa ukosefu wa shahada huku ikiwa hatujajenga vyuo vya kutosha?

Sababu yangu ya pili ambayo pia imeshikamana na ile ya kwanza ni kwamba katika yale majukumu ya MCA ambayo ni uwakilishaji, utungaji sheria na uangalizi/oversight, sioni lile ambalo lina lazima ya shahada.

Uwakilishaji ni kuchukua maoni na matatizo ya wananchi na kuyafikisha katika ofisi husika. Jukumu hilo halina lazima ya shahada.

Katika utungaji wa sheria, ni wabunge wachache sana ambao wana ufahamu na uwezo wa kutunga sheria. Wabunge hupeana maono yao kwa wana sheria na wataalamu hao ndio hufanya ile shughuli ya utunzi. Halafu Wabunge wakaijadili na kuipitisha au kuipinga ile sharia baada tena ya kupata maoni kutoka kwa wananchi kupitia public participation. Hapo sioni lazima ya shahada.

Katika jukumu la uangalizi/oversight MCAs hutegemea pakubwa ripoti za Mhasibu Mkuu na Wahandisi. Jukumu la uhasibu au uhandisi sio lao.

Kwangu mimi sioni kwa nini wagombea hao walazimishwe kua na shahada ya chuo kikuu. Cha muhimu ni wawe wanaweza kusoma na kuandika kwa kutumia lugha za kiingereza na Kiswahili – basi.

Mwisho tusisahau kwamba Kenya hii ni yetu sote yaani wale walio bahatika kusoma na hata wale ambao hawajabahatika kusoma. Sote tuna haki ya maisha kwa hiyo sio vyema kufungia wengine nje bila kuwa na sababu maalum.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago