Categories: Taita Taveta News

MHESHIMIWA MDUMIKI ADIDIMISHA NYOTA YAKE YA KISIASA KWA MATAMSHI YA KUSISIMUA

 

Katika hafla ya hivi majuzi iliyoandaliwa kwa heshima ya wakaazi wa Taita Taveta wanaotoka maeneo ya Kaskazini mwa Kenya, Mheshimiwa Peter Shake, almaarufu Mdumiki—ambaye pia ni Canon katika Kanisa la ACK—aliwashangaza wengi kwa hotuba yake ya kusifu na kuhamasisha jamii ya Cushites kujitokeza katika siasa za kaunti.

Mdumiki, baada ya kimya kifupi cha kutafakari, aliamua kutumia jukwaa hilo kuwapongeza jamii hiyo kwa bidii yao katika biashara na ujenzi wa taifa. Zaidi ya hapo, aliwahimiza kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao kwa kusimamisha wagombea wao kwa nyadhifa mbalimbali, ikiwemo MCA, Seneta, Mwakilishi wa Wanawake, Gavana, na hata Ubunge.

Hata hivyo, matamshi haya yameibua mjadala mkali. Baadhi ya wakaazi wameyachukulia kama usaliti wa kisiasa, hasa ikizingatiwa kuwa Mdumiki alipigia kura ya “NDIYO” Mswada tata wa Finance Bill 2024 uliowakera Wakenya wengi. Kauli moja mitandaoni ilisomeka:

“Pengine Mdumiki anajua ile YES yake itampeleka nyumbani, sasa anataka viti vichukuliwe na wachia mbai!”

Fununu kuwa anaandaa kuwania kiti cha Ugavana mwaka 2027 zimezidi kuchochea mjadala, huku wengi wakijiuliza: Je, matamshi haya ni mkakati wa kujijenga kitaifa au ni kaburi lake la kisiasa?

Katika siasa, kila neno huweza kugeuzwa kuwa silaha au daraja. Mdumiki anasalia na jukumu la kuwasiliana kwa hekima na kuunganisha jamii zote—kama kweli anataka kuendelea kupanda ngazi za uongozi.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

5 hours ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

8 hours ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

1 day ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

2 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

4 days ago

TAITA TAVETA: WE CANNOT CONTINUE THIS WAY — A COUNTY GOVERNMENT IN CRISIS OF ACCOUNTABILITY

Kwaela News Network | Editorial Taita Taveta County is confronting a governance crisis that can…

6 days ago