Categories: Voice of Reason

MFAHAMU BINADAMU ALIYEKUBALI KUTAFUNA VICHUNGU MISITUNI ILI MABEBERU WATAFUNE VINONO MTAANI!

Na Denis Mpagaze

Ni Joseph Kony aliyezaliwa katika nchi iliyobarikiwa watu wa ajabu akiwemo Idd Amin na Joseph Kibwetere; Kibwetere ni yule Mchungaji aliyewatia kiberiti waumini wake waliokuwa wakimlaumu kwa kuwadanganya eti ni mwisho wa Dunia, akawachoma ili kupunguza kelele; naizungumzia Uganda, nchi ya Yoweri Museveni na familia yake, nchi ambayo haijawahi kuona marais wake wakiingia Ikulu kwa kupokezana vijiti kwa amani kama Tanzania zaidi ya mtutu wa bunduki na mapinduzi ya kijeshi; nchi ambayo bila ubabe huwezi kuitawala; hata Museveni amefanikiwa kwa sababu alitumia ubabe wa Kony kujiimarisha kijeshi na kiuchumi kwa silaha alizonunua kumshughulikia Kony zikaenda kuishughulikia Congo DRC!

Halafu ubabe wa Joseph Kony siyo maigizo kama ya wanywa pombe za ukubwani,huyu brother ubabe wake ni wa kuzaliwa nao; siku amezaliwa tu, dogo alisimama ghafla mithili ya kitoto cha mbuzi kinachozaliwa na kukimbia wakati huohuo, mama yake akasema “Mungu katuletea balaa” na kweli Kony akawa balaa kuanzia nyumbani hadi nje ya Uganda, Marekani wakamuita Gaidi wa Dunia kuwahadaa wajinga na wakati wenye akili tunajua kabisa wao ndo wanamlinda pamoja na fujo zake kwa sababu palipo na vurugu kuna ulaji wa Marekani; kama huamini nionyeshe sehemu yenye vurugu Duniani isiyokuwa na mkono wa Marekani! Hivi unataka uniambia Museven, Bush na Obama walishindwa kabisa kumkamata Kony na kumuua? Ina maana Kony ana nguvu kuliko Sadam Hussein na Muammar Gadaffi waliokaangwa kama chips kuku huku Dunia ikishuhudia?

Leo ukilitaja jina la Joseph Kony unaona watoto wadogo wanabakwa, watoto wadogo wanaua wazazi wao, watu wasiokuwa na hatia wanakatwa masikio, wanakatwa lipsi za midomo kuacha meno nje mithili ya muhuni anayejichekesha pasipo sababu; nakwambia ukilitaja jina la Kony utaona watu wakitobolewa macho kwa sababu wamekataa kumuunga mkono, utaona nyumba zikichomwa moto; lakini kamwe hautaona silaha anazotumia Kony zinatoka wapi, wala huwezi kujiuliza silaha anazopata Museven kutoka Marekani kwa ajili ya kumsaka Kony zinafanya kazi gani maana zimeshindwa kumkamata Kony; nasema hivi huwezi kuyaona hayo kwa sababu Wajinga ndo wanaotafunwa kama mishikaki ya Chato! Kwani aliyetengeneza filamu ya kuonyesha ushenzi wa Kony ni nani? Itafute uone inavyotisha. Inaitwa Invisible Child: Discover the Unseen! Yaani ukiitazamana utadhani watu wa Kaskazini Uganda wanakula na kunywa vita, kumbe propaganda za wahuni.

Aliyeshambuliwa na wanamgambo wa LRA

Halafu siku chache baada ya Jason Russell kutengeneza filamu hiyo akawa chizi, tukasema Kony amemloga maana aliona wamemdhalilisha na wakati wao ndio walimfadhili kufanya huo ushenzi, lengo wapate upenyo wa kuja kuiba mafuta kwa jina la kumsaka gaidi wa Dunia! Baada ya kujitekenya kwa filamu hiyo Marekani ikaingia msituni kumsaka Joseph Kony aliyezaliwa mwaka 1961, Obama akatangaza hadi dau la dola milioni tano kwa atakayetoa taarifa anakojificha Kony na wakati wanajua aliko! Hivi wazungu wanatuonaje sisi?

Hivyo ndivyo Filamu hiyo ilivyosaidia kulikuza jina la Joseph Kony, mtoto wa katekista ndani na nje ya Afrika hadi Marekani ikamtunuku ugaidi wa Dunia. Wazazi wake walimtumikia Mungu yeye akamtumikia Shetani na jamaa zake mabeberu. Baba yake alikuwa Katekista wa kanisa katoliki, mama yake muangilikana swafi lakini dogo akaja kuwa mganga wa kienyeji. Sijui kwa nini watoto wengi wa watumishi wanakuja kuwa kenge baadaye? Kony alitoka kanisani akiwa na umri wa miaka 15, akaingia kwenye uganga wa kienyeji. Halafu hata kuwaita matabibu wetu waganga wa kienyeji ni kujidhalilisha. Hawa siyo waganga wa kienyeji, hawa ni madaktari nguli ndo maana tiba za kizungu zikidunda tunakimbilia kwao. Utasikia jaribu tiba mbadala. Ebo! Eti tiba mbadala! Tiba zetu tunaziita mbadala. Tunafail sana Wakushi! Tiba zetu ni halisi na za kizungu ndo mbadala. Hadi leo Kony anawatibu watu wake kule msituni kwa mitishamba na wanapona halafu wewe unaziita mbadala. Shindwa!

Halafu akili za Joseph Kony alizijua yeye mwenyewe maana hata shule aliachana nayo kama kawaida ya watu wenye akili nyingi ingawa walimu huwaona chenga. Tatizo la walimu wetu huwapima watoto kwa kipimo cha samaki kupanda mti akishindwa anaitwa mjinga. Bora hata Wanyamwezi wanaopima uzima wa kuku mgonjwa kwa kumpaka pilipili sehemu ya haja kubwa ili mnunuzi asishtukie kama kuku ni mgonjwa kutokana na uchangamfu anaouonyesha kwa muwasho wa pilipili kuliko walimu wa siku hizi. Hii dunia inatawaliwa na watu wenye akili sana. Tuanzeni mazoezi ya kutumia akili, inalipa sana! Hata watu wengi walioacha alama hapa duniani iwe nzuri au mbaya walitumia akili zao vizuri kwa kukataa kupimwa kwa mitihani ya darasani. Idi Amin aliishia darasa la nne akawatoa jasho hadi wazungu, Adolf Hitler aliogopa hadi mitihani ya darasani lakini akaitikisa Dunia, Bill Gates aliacha shule na kutengeneza Microsoft inayokurahisishia kuchepuka, hata Mark Zuckerberg aliishia njiani baada ya kuona Facebook aliyotengeneza inafanya makubwa kuliko walimu wanaomfundisha; sasa wewe jaribu kuacha shule uone maisha yatakavyokunyoosha maana huko kwenu mkiachaga shule mnashinda vichakani wakiiba mazao ya watu kama ngedere.

Yoweri Museveni

Pengine Kony angeendelea na masomo asingeangukia kwenye mtego wa kuteseka maporini kwa faida ya wajanja. Safari yake kuelekea kuishi misituni ilianza siku ile Yoweri Museveni ampindue Rais Tito Okello na kuendeleza mashambulizi Kaskazini mwa Uganda. Lengo lake ilikuwa kuvunja nguvu ngome hiyo yenye historia kubwa ya kijeshi nchi Uganda. Hata Jenerali Idd Amin alitoka huko. Hata Jenerali Tito Okello aliyempindua Milton Obote alitokea huko Kaskazini. Enzi za ukoloni watu wengi kutoka huko walijiunga na jeshi la mkoloni. Kumbe eneo la Kaskazini ndo lilikuwa tishio kwa Museven ndo maana ameshughulika nalo muda wote. Sasa basi baada ya kuona Museven anaendelea kuwaumiza watu wa Kaskazini, Kony aliamua kujiunga na vuguvugu la kumpinga Museven,vuguvugu lililoanzishwa na Bi Alice Auma!

Huyu Alice Auma alikuwa mganga wa jadi, akashukiwa na roho wa Lakwena, askari wa zamani akimtaka aachane na tiba akapambane na uovu wa Museven.Lakwena alimwambia mama kwamba haina maana unatibu watu kisha wanachinjwa na vikosi vya Museven. Mama akatii maelekezo ya Lakwena na kuanzisha vuguvugu hilo la Roho Mtakatifu. Katika mashambulizi yao ilikuwa ni mwiko kutumia silaha za moto badala yake walitumia fimbo na mawe kupamba na vifaru,mabomu na mizinga ya Museveni. Mama aliwaambia wapiganaji wake kujipaka mafuta ya nazi kuzuia risasi kwa sababu kuna nguvu katika nazi! Wazee wa zamani walitumia nazi kuondoa mikosi na balaa siyo kukwepa risasi za moto. Baada ya kunuia mabaya walipasua nazi njia panda na mambo yakawa shwari. Tunaita ushirikina ndo maana balaa haziishi. Prince Katega II anasema siku hizi hakuna haja ya kwenda njia panda kama unataka kuondoa balaa kupitia nazi. Badala yake unachukua karatasi, unachora alama ya msalaba kisha unapasua nazi katikati ya msalaba, mambo yanakwisha! Kuna balaa zinakusibu? Hebu jaribu kufanya hivyo then unipe jibu. Hata kama mume anakutoa jasho,pasua nazi tu uone kama ataendelea! Ila akikukuta mimi simo, atakuja kulimaliza Prince Katega mwenyewe! Huo ndio ulikuwa ukuu wa Afrika!

Alice alimtoa jasho Museven kwa muda mfupi lakini Museven akamuwahi. Siunajua tena Jenerali wa vita! Mama alipozidiwa nguvu alikimbilia zake Kenya. Akiwa huko Kenya aliendelea na shughuli zake za uganga, muziki wa Museven akamuachiaa Kony na wenzake. Siku moja mama akiwa Kenya alitangaza amepata dawa ya ukimwi lakini yeye akaja kufa kwa ukimwi mwaka 2007 kwa sababu mganga hajigangi! Joseph Kony alishika usukani na kuendeleza vuguvugu la kupambana na Museven. Kony alivunja miiko ya kundi kwani alitumia silaha za moto, lakini pia akabadili jina la kundi likaitwa the United Holy Salvation Army na baadaye akiliita tena kundi hilo Uganda Christian Movement na mwaka 1992 Lord Resistance Army ilizaliwa rasmi kwa lengo la kuitawala Uganda kwa Amri Kumi za Mungu. Kony aliendelea kutumia mafuta ya nazi kama kinga. Aliwaamuru vijana wake kabla kuingia front kuchora alama ya msalaba kiufuani kwa kutumia mafuta ya nazi.

Kony alihakikisha kila mtu anashiriki kuikomboa Uganda, aliyekataa alikatwa masikio, midomo na mapua ingawa Kony anasema askari wa Museven ndo walikata watu. Wakati huo wote Kony alipata silaha zake kutoka Marekani. Unaona jinsi waswahili tunavyotumika? Yaani wakati Wazungu wanampatia silaha Kony kuhakikisha Museven hatawali,Museven naye alifadhili kikundi cha waasi huko Sudani, kikundi kiliitwa Sudanese People’s Liberation Army cha kina Garaang kuhakikisha Al Bashir hatawali Sudan na kweli Sudan ilikatika vipande viwili na kuzaa Sudan Kusini. Al Bashir kuona hivyo naye akaanza kumsuport Kony ili kummaliza Museven.

Omar Al Bashir

Mchezo wa Kony na Museven umedumu kwa zaidi ya miongo miwili sasa kila mmoja akifaidika kwa anavyojua ndo maana harakati zote za kumkamata Kony zimedunda. Nakumbuka March 1991 Museven alianzisha Operation North kumshughulikia Kony wakajifelisha. Badala yake zoezi hilo liliishia kuwaumiza raia wasioujua mchezo.Ni baada ya Museven kuwarubuni watu waliomsupport Kony kujiunga na Museven kupitia Arrow Groups alizozianzisha. Akawapa mishale na upinde kupigana na Kony. Kony akareact kwa kuwachinja waliojiunga na Museven kumsaliti. Kony aliwaua watu kwa refence ya Biblia kwamba hata Mungu aliwaua washenzi kwa gharika na moto wa Sodoma na Ghomora. Tatizo la Biblia unaweza kuitumia vibaya kuhalalisha ushenzi wako. Wakoloni walitumia Biblia kuhalalisha biashara ya utumwa. Hata Nabii Tito wa Tanzania alitumia Biblia kuhalalisha ulaji wa housegirls!

Kwa sababu Kony alijua kabisa yuko pale kwa maslahi ya Museven na Marekani siku zote alitamba hadharani kwamba hakuna atakayeweza kumuua. Sana atapotea kama Hitler. Ukitaka kuamini hawa watu wanatuchezea jiulize nani alimjengea nyumba nzuri mama yake Kony pale kijijini kwao hadi watu wa huko wakapaita state house; jiulize nani aligharamia mazishi ya kifahali ya mama yake Kony; nani aligharimia matibabu ya wazazi wa Kony? Nani aliwatunza wazazi wa Kony tangu Kony ahamie msituni? Kwa taarifa yako vyote vilifanywa na Museven! Sasa unaanzaje kusema Kony na Museven ni maadui? Hata ICC walipomtaka akajibu mashitaka 33 ya uhalifu wa kivita na uvunjifu wa haki za binadamu Kony aliishia kuongea kwa kejeli mbele ya vyombo vya habari kwamba hayuko tayari kufika mbele ya mahakama ya ICC kujibu mashitaka kwa kuwa hajafanya lolote baya. Kwanza aliwaambia hatuna watoto, tunawapiganaji tu,sasa nini kinawawasha? Alisema yeye ni freedom Fighter, muuaji ni Museven! Sikilizeni, ”

Waziri wa Nchi Bi Betty Bigombe bila kujua mchezeo wa Kony na Museven alijaribu kuwakutanisha Kony na Museven wayaongee yaishe lakini kilichotokea hana hamu. Bi Bigombe alisafiri hadi maporini alikojificha Kony baada ya kumuomba appointment. Kony alimpokea vizuri, wakateta ya moyoni,mama akarudi salama na kwenda kwa Mzee kumpasha habari njema ya Kony kuwa tayari kusemezana na Museven ana kwa ana kwazi kwake kupanga appointment. Badala ya Museven kupanga appointment waongee na Kony yaishe, Museven aliitisha Mkutano wa Hadhara na kumtishia Kony hadharani n kuwa ajitokeze mara moja la sivyo akabiliwe vikali na vikosi vya serikali. Vikosi vya Kony vikajibu kwa mashambulizi yaliyoua raia wasiokuwa na hatia .Bi Bigombe kuona hivyo akajizulu jukumu na kwenda zake Havard Marekani kusoma na sasa ameajiriwa Benki ya Dunia.

Kama Mabeberu wanavyowatumia Al-shabab, Alqaeda na makundi mengine ya kigaidi kujustify uvamizi wa nchi za watu kuiba rasilimali ndivyo Museven anavyomtumia Kony kwa maslahi yake. Leo zinatengenezwa propaganda za kijinga kututoa kwenye reli. Eti Joseph Kony anawake kibao, anapenda ndoa za mitaala, kwamba anawake zaidi ya 100 na watoto wa kumwaga.Hivi kweli mitaala Afrika ni kitu cha ajabu? Nani anaweza nionyeshe Mwafrika asiye na mitalaa ili tumpeleke kwenye jumba lamaonyesho! Zinaitwa nyumba ndogo na michepuko.Tena wakati mwingine unaweza kuta njia kuu yako ndo mchepuko wa jirani yako sema tu hujui na bora usijue na wala usitafute kujua ukatufia bure kwa presha. Sana unachotakiwa kujua ni kwamba hoja ya mitaala ya Kony siyo issue ya kuongelea mbele za watu wanaojielewa!

Sisi tunabaki kujadili jinsi Kony anavyoshughulikia wake 100, watu wanaendelea kuumia. Mwaka 2005 Kony na Museven walipanua himaaya yao hadi Sudan Kusini, Afrika ya Kati na Congo! Kony akatikisa nchi nne na wameshindwa kumnasa. How? Majeshi yenye majeneral wa kijeshi wanashindwa kumnasa Kony kabisa? Eti Desemba 2008, jeshi la Kongo, Uganda na Sudan, vilivamia mji wa Garamba ilikokuwa kambi ya Kony kwa lengo la kuwanyang’anya silaha lakini wakashindwa na sisi tukaamini hivyo.Hawa walienda kufanya vurugu Kongo tu ili wenye akili wapate mpenyo wa kuiba mali za Congo. Halafu katika uvamizi huo hata Marekani walikuwemo. Baada ya kushindwa Marekani akamtangaza kony kuwa Gaidi wa Dunia. Hivi tangu lini Marekani akashindwa kizembe hivyo? Baadaye Kony anajitokeza hadharani akidai analindwa na roho mtakatifu. Danganya toto. Ni kweli Kony anasali na kuswali, tena kwa bidii; anafunga ramadhani na kwaresma, anafanya ibada kwa miungu yake hana dini kamili, ramadan yupo, kwaresma yupo na katika funga zote anafanya ibada kikamilifu. Tangu utotoni alikuwa mcha Mungu, alikuwa muitikiaji, msaidizi wa kasisi madhabahuni.

Pamoja na bidii yake katika kuswali, kusali na kutambikia bado najiuliza inakuaje mtu kama Kony kuwa tishio Congo, Sudani, Afrika ya Katina uganda? Hapa lazima kuna nchi zitakuwa zinafanya ushenzi katika ardhi hiyo yenye utajiri na kuwasingizia waasi wa Kony Wanaidanganya Dunia kuwapatia silaha eti kumpiga Kony kumbe wanazitumia kuvamia Congo. Kwani waasi wa Congo wanatoka wapi? Nani anawafadhili? Congo yote imejaa silaha na damu! Iko hivi,silaha zinanunuliwa kumpiga Kony lakini zinapiga DRC!

Uganda Defence Force wakiwa kwa mazoezi

April 2017, Ugandan na jeshi la Marekani walitangaza rasmi kuacha kumuwinda Kony. Kwamba Kony siyo tishio tena Uganda. Issue siyo kwamba Kony si tishio tena, issue ni kwamba Kony hakuwa muasi. Niambie katika dunia ya leo ni wapi serikali inasumbuliwa na waasi kwa miaka zaidi ya 20 bila kuwatia nguvuni? Ukiona kikundi cha waasi kisicho na kikomo ujue kipo kwa interest za watu tu basi.Anzia huko DRC ambako vita haiishi zile ni interest za watu. Waasi ni akina Savimbi walioalikamatwa na kuawa. Hawa wengine ni mali ya Museveni kuwapumbaza Waganda kwamba waendelee kumuamini yeye ndo anawaweza. Siku rais Museveni akiondoka madarakani ndiyo utakuwa mwisho wa Kony na genge lake. Kony na Museven ni mradi wa Marekani kama ilivyo Al Kaida na Osama. Kwani lengo la CIA kutengeneza Al qaeda ni nini? Vp Al shabaab je? Hata Osama walimtengeneza wao kwa lengo la kuudhoofisha ulimwengu wa kiarabu!

Museven anapeleka jeshi Somalia akimuacha Kony kwa sababu anatumia sababu ya vita hiyo kuendelea kufanya manunuzi makubwa ya vifaa vya kijeshi. Leo Uganda ni moja ya nchi yenye majeshi bora Afrika Mashariki. Utakumbuka wakati msiba wa Nyerere, Museveni alileta dege kubwa ambalo hata jeshi letu halina kwa ajili ya kusafirisha waombolezaji kutoka Dar kwenda Musoma. Sijui kwa nini Waafrika kila tunapotegwa tunanaswa.

Hata Gaddafi alinaswa baada ya kudhani ni rafiki mkubwa wa Berlusconi, Tony Blair na Sarkozy.

Nyerere aliwahi kutoa mfano wa kisa cha shoka na mpini, ambapo shoka bila mpini lilikuwa haliwezi kufanyakazi, lakini siku mti ulipojitokeza kumsaidia shoka kuwa mpini, ndipo miti ilipoanza kuathirika.

Tafuteni ukombozi wa Fikra na mengine tutazidishiwa anasema Denis Mpagaze,mwandishi wa kitabu cha Wasomi Huru na Ukombozi wa Fikra.

Rusha elfu kumi kwa +255753665484 akurushie kwa Whatsapp!

Viko katika soft copy! 

Mungu Ibariki Afrika!

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago