Mbunge wa Taveta Mheshimiwa Dr. Naomi Shaban
Mbunge wa Taveta Dkt. Naomi Shaban amepongeza hatua ya serikali ya kaunti kununua mashine ya kuchimba maji na kuitaja hatua hiyo kama itakayosaidia pakubwa kukabiliana na uhaba wa maji. Naomi amesistiza kuwa ipo haja ya viongozi wa kitaifa na wale wa kaunti kuzidi kushirikiana ili kuafikia maendeleo na kuomba wananchi kuunga mkono juhudi za viongozi wao.
“Tangu mwanzo tuliapa kufanya kazi na gavana aliyechaguliwa na tunaona ameleta mashine ya kuchimba maji. Shida kubwa tuliyonayo hapa ni uhaba wa bidhaa hiyo na hatua aliyochukua itasaidia pakubwa kukabiliana na changamoto hiyo. Tunaunga mkono juhudi zinazowekwa kutatua changamoto kuu zilizopo.” Dkt. Naomi Shaban amesema.
Ameomba wananchi haswa wakulima kujitokeza kwa wingi wakati wa mafuzo ya ukulima ili wapate nasaha itakayowasaidia kuimarisha sekta ya ukulima wakati huu mashine hiyo imepatikana kwani itasaidia pakubwa kuongeza mazao ya shambani.
“Hivi majuzi serikali ya kaunti ilianzisha mafunzo ya faragha ya ukulima na ufugaji. Naomba wananchi mjitokeze kila yanapoandaliwa na tukumbatie kilimo biashara ikizingatiwa kwa sasa tumepata mashine hii.” Ameongeza
Gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja amesistiza haja ya viongozi kutekeleza miradi ya maendeleo pasipo kuingiza siasa na kuongeza kuwa muda wa siasa ulipita na niwakati wa viongozi kufanyia wananchi maendeleo.
“Mapema mwakani, rais Uhuru Kenyatta atazuru kaunti hii kuzindua mradi mkubwa wa maji ya Mzima II. Langu ni kuomba tuzidi kushirikiana kwa manufaa ya mwananchi na tuwache siasa za 2022 kwa sababu hiyo itafika na ipite ila kwasasa tutekeleze wajibu tuliopewa na mwananchi.” Gavana Samboja amesema.
Haya yanajiri huku bunge la kaunti likiombwa kutenga fedha za kutosha kwenye bajeti ya ziada ili waweze kununua vifaa zaidi vya kutengeneza/kuimarisha miundo misingi ikiwemo barabara na mabawa ya kuvuna maji ya mvua.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment