Categories: Academics

MASAIBU YA SHULE YA UPILI YA MLAMBA – MRUGHUA

Shule ya upili ya Mlamba Secondary School ilioko Mrughua, kaunti ndogo ya Mwatate imekumbwa na masaibu kadha wa kadha.

Baadhi ya matatizo hayo ni kama yafuatavyo.

Viwango vya elimu kudorora.

Ijapokuwa shule hii ya upili iko kulomita mbili kutoka shule za msingi, Mwavunyu na Mrughua, zinayosifiwa kwa kuwa na matokeo bora zaidi katika mitihani ya darasa la nane, Mlamba ni moja ya shule zinazopata matokeo duni katika mtihani wa KCSE.

Upotovu wa nidhamu.

Imeripotiwa kuwa shule hii ina visa kadha wa kadha vya wanafunzi kukosa nidhamu.

Inasemekana kuwa baadhi ya wanafunzi wamejiingiza kwa anasa na uraibu wa kiholela. Kuna wanafunzi wamepatikana wakitumia madawa ya kulevya kama Bangi, Miraa na hata ugoro. Wanafunzi hao huenda wakaishia kutumwa manyumbani kwa muda fulani (suspension) na hivyo basi kupoteza muda mwingi na kuadhiri masomo yao.

Matokeo ya KCPE ya 2021

Matatizo ya karo

Baadhi ya wanafunzi wanatoka kwa familia zisizojiweza kihali na mali, hivyo basi kusababisha wanafunzi hao kutumwa manyumbani sababu ya matatizo ya Karo ama Ada zinginezo zinazo itishwa shuleni. Katika kikundi cha WhatsApp cha Mrughua Highlands Mwalimu mkuu anadai kusaidia wanafunzi kadhaa kupata Bursaries. Mwalimu huyo huyo hataki kabisa kujadili matokeo kwa ujumla, na haswa kuyalinganisha na matokeo walio pata KCPE ili kuthatmini kama Kuna walio ongeza alama ama kupunguza. Cha kusitikitisha mno ni kuwa mijadala hii inanuiwa kusaidia shule kwa ujumla kuimarika.

Wanafunzi kukosa motisha wa kufanya bidii masomoni.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wanafunzi hawatilii elimu maanani. Kuna fununu kuwa kuna wanafunzi wamejizatiti kupata hela za kununua bodaboda zao wenyewe na wanafanya biashara, ila kujilipia karo ya shule hawataki kabisa.

Mwalimu mkuu mwenye kiburi

Inadaiwa kuwa Mwalimu mkuu wa shule hii amekaa sana kwenye shule hii mpaka ameanza kuonyesha kiburi wazi wazi. Kiburi hiki amekihidhirisha hadharani kwenye kikundi cha Mrughua Highlands ambapo hukataa kanisa kujibu maswali ama kujibu na madharau. Rekodi za matokeo ya KCSE zinaonyesha wazi kuwa tangu aingie huko, kama mwalimu mkuu, matokeo ya KCSE yamekuwa yakidorora.

Isitoshe, mwalimu huyo mkuu akiulizwa maswali kwenye kikundi hicho anadai anachafuliwa jina mtandaoni na anatishia kushitaki wanaomuuliza maswali.

Haya na matatizo mengine yametuma elimu katika shule hii kuwa ya chini kabisa.

Isisahaulike kuwa wengi wa wanafunzi wanaosomea katika shule hii walifanya vizuri katika mitihani ya KCPE ila ikifika kwa KCSE wanapata D na E.

Wazazi na wakaazi wanaiomba idara ya elimu na viongozi husuka waingilie kati kurekebisha matatizo haya.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago