Categories: Academics

MANOA SECONDARY SCHOOL: WAZAZI WACHIMBA VYOO, PESA ZA SHULE ZAPOTEA, VIONGOZI WALAUMIWA

Baada ya kuangazia hali mbaya ya vyoo katika Shule ya Sekondari ya Manoa, duru mpya zinaibua picha ya shule inayokumbwa na msururu wa matatizo makubwa ya usimamizi.

Kwa sasa, wazazi wamechukua jukumu la kujichimbia vyoo baada ya shule kushindwa kutatua tatizo hilo kwa muda mrefu. Hata hivyo, matatizo hayakomei hapo. Shule haina ua (fence), hali inayohatarisha mali ya shule kutokana na wizi, mifugo na wanyama pori. Tayari, mitungi ya gesi imeripotiwa kuibwa na hadi leo haijarejeshwa.

Inadaiwa kuwa wizi huo ulichangiwa na giza, baada ya uongozi wa shule kuamuru taa zisizimwe usiku ili kupunguza gharama za umeme.

Masuala haya yaliwasilishwa kwa ofisi ya NG-CDF Mwatate, ambapo shule iliombwa ichague kipaumbele kimoja kati ya: basi la shule, vyoo, ua au maabara ya kisasa. Kupitia kura, kamati ya shule ilichagua modern laboratory kuwa kipaumbele. Hata hivyo, duru zinasema NG-CDF inalazimisha ufadhili wa basi la shule, kinyume na uamuzi wa kamati.

Wakati huohuo, licha ya wazazi kulipa karo, shule inadaiwa kukosa fedha za matumizi ya msingi. Walinzi, wapishi na walimu wa PTA hawajalipwa kwa zaidi ya miezi minne. Wazazi sasa wanataka akaunti ya shule ichunguzwe kubaini pesa zinakoelekezwa.

Maswali zaidi yanaibuka baada ya shule kufanikisha safari ya wanafunzi kwenda Nairobi kwa Tamasha la Muziki (Music Festival) kwa gharama inayodaiwa kuzidi shilingi nusu milioni, huku shule ikibana matumizi muhimu kama umeme na usalama. Wadadisi wanasema juhudi hizi ni za kujenga taswira ya nje, ilhali ndani shule inaoza.

Walimu pia wanalalamika kulazimika kutumia pesa zao binafsi kugharamia michezo na shughuli za wanafunzi, wakiahidiwa kurejeshewa bila mafanikio.

Wazazi na wadau sasa wanatoa wito kwa viongozi wa elimu, NG-CDF na mamlaka husika kuingilia kati mara moja, kufanyika kwa ukaguzi wa kifedha na kurejeshwa kwa nidhamu ya matumizi ili kulinda maslahi ya wanafunzi.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago