Categories: Reviews

MANIFESTO YA GAVANA GRANTON SAMBOJA YA MWAKA WA 2017

KURA KWA GRANTON SAMBOJA NI KURA AMBAYO:-

Itaniwezesha kuwa kiongozi anayetumikia watu wake kikamilifu.

UONGOZI BORA ZAIDI

Hii ni kura itakayo badilisha uongozi ulioko wakati huu na kuketa uongozi bora zaidi.

ELIMU

Kura yako itahakikisha utoaji wa elimu hadi chuo kikuu kwa wanafunzi wote, utoaji wa misaada zaidi ya masomo ama bursary sambamba na elimu bora zaidi kwa watoto wetu. Nitahakikisha kuna taasisi zilizoimarika za elimu kutimiza mahitaji yetu katika county yetu.

VIFAA VYA KUTOSHA

Tutahakikisha kuna vifaa vya kutosha kwa shule zinazotoa mafunzo mbali mbali ya kikazi ili kuongeza ujuzi na maarifa ya watu wetu.

TAMADUNI

Tutadumisha na kuhifadhi utamaduni wetu.

DINI

Nitahakikisha dini zote zinaheshimiwa.

MAZINGIRA

Nitahifadhi na kudumisha mazingira.

MAJI

Kura yako itaniwezesha kuleta maji ya mfereji karibu na kila nyumba.

KUNYUNYUZIA MASHAMBA

Itaniwezesha kuleta maji mtakayotumia kunyunyuzia mashamba yenu, maji kwa mifugo wetu na pia wanyama wetu wa pori.

UFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

Nitaanzisha mradi kabambe wa kuboresha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

KAMPUNI YA NYAMA

Nitazindua kampuni ya nyama – Taita Taveta Meat Commission

MAZIWA

Nitazindua kiwanda cha maziwa.

KILIMO BIASHARA

Nitaboresha kilimo cha kibiashara sawia na kutoa kandarasi kwa wakulima watakaouza mazao yetu katika nchi za ng’ambo.

KUINUA PATO

Nitafanyab kila niwezalo kuinua pato la kila mmoja wenu na familia zenu.

NYUMBA

Nitahakikisha kumejengwa nyumba bora za makaazi katika County yetu.

MATIBABU

Nitatoa vifaa na madawa ya kutosha kwa vituo vyote vya matibabu.

MUUNDO MSINGI

Nitajenga barabara na kuimarisha muundo msingikatika kila lokesheni.

VIWANDA

Nitaanzisha viwanda vidogo vidogo katika kila lokesheni na viwanda vikubwa Voi, Mwatate, Wunfanyi na Taveta.

UCHIMBUAJI MADINI

Nitaanzisha vyama vya ushirika miongoni mwa Vijana katika sekta ya uchimbuaji madini.

WAFANYI BIASHARA

Nitafungua nafasi zaidi za kufanya biashara na kuwapa misaada ya kifedha wafanyi biashara wetu.

KINA MAMA

Nitainua maisha ya kina mama kiuchumi kupitia uanzishaji wa masoko kwa mazao yetu.

VIPAWA NA TALANTA

Nitafanya juhudi zote katika kuinua vipawa na talata za vijana wetu katika fani za kandanda, riadha na uimbaji.

Hatimaye tumepata kiongozi

Kwaela News Network

Leave a Comment

View Comments

Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago