Categories: Opinion

MAMA MBOGA NA WALALAHOI TAITA TAVETA WAHOFIA KUANGAMIA – JE SAMBOJA YUPO?

 

Mbwa akiuma MTU hiyo siyo habari lakini MTU akiuma MBWA hilo sio la kawaida na ni HABARI za kushangaza na kila mtu angependa kusoma ili aelewe!

Kwa miaka mwenyezi Mungu aliyonipatia duniani mpaka hivi sasa, na simichache, nimeona na kushuhudia mengi mazuri, mabaya, yamauthi, ya kero nakadhalika. Na kati ya yote, hakuna la kero kama mtu aliyepatiwa jukumu la kutekeleza wajibu fulani basi kutaka wasifa kwa kutekeleza wajibu wake kulingana na maagizo, sheria, matarajio na takrimu zote.

Mfano ni kama Baba mzazi anaporudi jioni nyumbani kwake amebeba lishe au ameleta pesa za kukimu mahitaji ya jamii yake, hilo ni jukumu na taraji la jamii kwake yeye kama mzazi na hakuna mwengine pasi yeye aliyetarajiwa kushugulikia mahitaji na maslahi ya jamii yake.

Iwapo mtu mwengine atatekeleza jukumu la huyo Baba pasipo yeye mwenyewe, hilo sio jambo la kawaida bali ni ukarimu na utu wa hali ya juu unaostahili kujulikana kote na shukrani kocho kocho kumiminiwa aliyetenda tendo hilo la ukarimu.

Serikali inapotoa huduma kwa watu walioidhamini hiyo serikali kwa kuipigia kura katika uchaguzi, hilo ni jambo la kawaida linalofanyika kupitia kwa kodi anayotozwa mwanachi, basi hilo ni jambo linalotarajiwa na mwananchi ususan kwa wakati unaofaa.

Hivi karibuni katika mitandao ninaona jarida mbali mbali kutoka tahasisi tofauti tofauti za serikali ya Taita Taveta zikitoa habari tofauti tofauti kuhusu yale mamefanya ama wanafanya kuhusu miradi mbali mbali katika kaunti yetu. Hilo japo ni lakutia moyo pia tunajiuliza, je walikuwa wakitarajia ni nani atafanya hayo na wao ndio waliochaguliwa na wakusanyaji wa kodi zetu?

Lakusikitisha ni kuwa mpaka hapo jana jioni tarehe 25 March, 2020, wakati dunia nzima inapambana na janga la ugonjwa wa “KORONA” hapa kwetu mazungumzo yalikuwa juu jaa miradi kama kuchimbua mitaro ya maji huko Mata – Taveta, ujenzi wa kiwanja cha mpira huko wadi ya Kaloleni  nakadhalika huku soko za wiki zikipigwa marufuku na serikali ya kaunti bila mikakati mbadala vile wachuuzi na wanunuzi watapata nafaka zao.

Viongozi wetu wameadimika sana hasa wakati huu dunia na taifa zima wanapambana na hali hii ngumu isiyo ya kawaida ya kujaribu kuzuia mchiripuko wa ugonjwa hatari wa “KORONA”. Je tunapomkosa Gavana wetu Samboja kutuongoza na kutupatia maelezo kama vile magavana wengine nikumaanisha kuwa yeye yuko na shughuli za muhimu kuliko Rais wa Taifa Uhuru Kenyatta ambaye hupata muda wa kuhutubia taifa na kutupatia tumaini na hakikisho?

Je Gavana Samboja yupo? Ikiwa hili janga la hatari ya “KORONA” linalo hatarisha maisha ya wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta sio muhimu kwake,  je ni nini kilicho na muhimu kwa Gavana Samboja? Wakati gavana anapotuma naibu wake kwenye kituo cha radio kueleza mikakati serikali yake imeweka ni kumaanisha labda gavana anauguzwa?

Wakati wa majanga kama haya hata katika Nyumba zetu, kila mmoja humtazamia Baba kutoa muelekeo na Baba anapoonesha kutokuwa na suluhu au tumaini, basi watoto huanza kuangalia pahala mbadala panapoweza toka suluhu.

Serikali ya kaunti, ni wakati mzuri waweze kuweka mikakati jinsi waendeshaji wa boda boda, mama mboga, wafanyi kazi wa mjengo, na wananchi wenye pato la chini wenye kutegemea kazi za siku kimaisha, vile watasaidika kwa wakati huu na siku zijazo ambazo zitakuwa ngumu sana. Hayo ndiyo mwanachi anataka kusikia na sio mitungi yenye nembo ama chapa kutoka kwa viongozi wa tabaka mbali mbali kana kwamba kaunti iko katika hali ya kampeni!

Habari tunazotarajia kutoka kwa viongozi wetu ni MIKAKATI YA KESHO KWA WAKESHO, WANJIKU, NASHERA NA WALALAHOI, vile watakavyo lidwa na kaunti yetu!

Geoffrey Kimonge Mbogo

Leave a Comment
Share
Published by
Geoffrey Kimonge Mbogo

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago