Gavana Samboja aahidi kuilinda ardhi ya Taita Taveta
Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imepinga umiliki wa shamba la ekari 900 ambalo linadhibitiwa na Idara ya Magereza katika wodi ya Bura gatuzi ndogo ya Mwatate. Serikali imesema ni sharti ardhi hiyo igawanywe kwa vipande vitatu (3) ili kuifaidi serikali, idara hiyo na mwananchi.
Akiongea alipoongoza shughuli ya kupeana hati miliki za ardhi katika wodi hiyo, gavana Granton Samboja amedokeza kuwa wataanza majadiliano na idara hiyo huku akipendekeza kuwa magereza yanafaa kutengewa angalau ekari 200.
Samboja hata hivyo ametoa tahadhari kwa wavamizi wa ardhi ambao wanalenga kuzuru eneo hilo wakidai kuwa wao ni waekezaji na kusema katu hatokubali mwananchi wake kudhulumiwa kutokana na raslimali anayomiliki.
Gavana aidha ameongeza kuwa serikali yake inaendelea na mikakati kuhakikisha inashughulikia swala la uskwata hivyo kuwataka wote watakaopata vyeti hivyo kujiepusha na kuuza mashamba na kuvitaja kama vitakavyowakwamua kutoka kwa umasikini.
Kwenye hafla hiyo, Samboja amewataka wakulima kutohofia kuchukua fursa hii ya mvua kupanda vyakula kutokana na mdudu aina ya kiwavi kwani idara ya Ukulima, Ufugaji na Samaki itaanza rasmi ziara za mashinani kutoa huduma kwa wakulima.
Waziri wa ardhi Bi. Claris Mnyambo ni miongoni mwa walioshuhudia zoezi hilo na amepongeza hatua ya akina mama wengi waliokabidhiwa vyeti hivyo. Vile vile, amewataka wananchi kutembelea ofisi husika wanapokumbwa na mizozo ya ardhi.
By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…
The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…
The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…
Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…
Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…
During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…
Leave a Comment