Categories: Taita Taveta News

MAANDAMANO ZIDI YA WANYAMA PORI RONG’E YASITISHWA NA MAOFISA WA USALAMA

Waakazi wa wadi ya Rong’e eneo Bunge la Mwatate wameshiriki maandamano kwenye barabara kuu ya Mombasa – Nairobi wakilitaka shirika la kudhibiti wanyamapori KWS kuingilia kati mzozo kati yao na Simba ambao kwa miezi tatu sasa wameua mifugo takriban 350, huku juhudi za kusaka fidia kwa waathirika zikiambulia patupu.

Alex Mwawughanga, Mzee wa Kijiji cha Rong’e nyika anasema hofu yao kwa sasa ni kwa wanafunzi ambao wameratibiwa kufungua shule juma lijalo, akisema maisha ya watoto wao yamo hatarini kwani Simba hao wanazurura mtaani bila ya woga.

“Takriban mifugo 350 wameangamizwa kufikia sasa, juhudi za kulifikia shirika la KWS zimeambulia patupu na boma zinazidi kusafishwa. Tunachoomba ni kudhibitiwa kwa Simba hawa kwakua shule zinafunguliwa na hatuna hakikisho kua watoto wetu wako salama.” Mwawughanga ameeleza.

Baadhi ya waandamaji Voi

Usemi wake ulitiwa uzani na bwana  Danson Kisombe, ambaye amekiri kupoteza mbuzi zaidi ya kumi kwa usiku mmoja hali anayosema huenda ikachangia kuongezeka kwa viwango vya umaskini eneo hilo ambalo tayari linakumbwa na baa la njaa kutokana na makali ya ukame.

“Kero hili huenda likatuwacha maskini kwakua tulitegemea sana mifugo ili tujikimu kimaisha ila sasa hali zimegeuka. Hatupo tayari kuchukua sheria mkononi, cha mno ni kwa shirika la KWS kudhibiti wanyama wao.” Amesema.

Hata hivyo juhudi zao za kutaka kuwasilisha lalama zao kwa afisi za KWS mjini Voi ziligonga mwamba baada ya maafisa wa usalama kukatisha maandamano hayo kwa kile walichodai ni kukosa kibali husika. Bernstein Sharry ni OCPD wa kituo cha polisi cha Voi.

“Jukumu letu kama maafisa wa usalama ni kuhakikisha sheria inafuatwa. Tunaufahamu kwamba ombi lenu kutaka kuandaa maandamano haya halikukubaliwa na sasa mkutano huu sio halali, tafadhali tufuate sheria inavyofaa.”

Haya yanajiri siku Moja baada ya uongozi wa kaunti hiyo ngazi ya serikali kuu na ile ya kaunti wakiongozwa na Gavana Andrew Mwadime kuandaa kikao na Waziri wa usalama nchini Kindiki Kithure ambapo swala la mzozo kati ya binadamu na wanyamapori liligusiwa.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago