Categories: Academics

Kaunti ya Taita Taveta iko tayari kwa ufunguzi wa taasisi za elimu – Waziri Makoko asema.

Utashi wa kuafikia vigezo vya wizara ya elimu na ile ya afya nchini kabla ya ufunguzi wa taasisi za elimu umezidi kushika kasi kaunti ya Taita Taveta, changamoto kwa sasa ikielekezwa kwa usimamizi wa vyuo vya anwai kuongeza juhudi zake za kuhakikisha vyuo hivyo vinafunguliwa tena punde tu wizara ya elimu itakaporidhiana kuhusu mdahalo wa ni lini shule zitakapofunguliwa tena.

Akitoa hisia zake kufuatia taarifa ya wizara ya elimu nchini kuhusu waalimu kurejea shuleni siku ya jumatatu kupanga mikakati ya ufunguzi, Waziri wa elimu, maktaba na vyuo vya anwai kaunti hii Daniel Makoko ametaka vyuo vyote vya ufundi kuhakikisha vinazingatia usafi wa mazingira kwa kuzikinyunyiza dawa mara kwa mara, kudumisha usafi kwa kuhakikisha maji safi yanapatikana kwa wingi shuleni pamoja na kuweka mikakati ya jinsi wanafunzi watakapoendelea na masomo pasi na kukaribiana.

Usemi wake umewekewa uzani na afisaa wake mkuu Simon Mwachia.

“Tumeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha wanafunzi, waalimu na kila mmoja yupo katika mazingira huru ya kumlinda dhidi ya msambao wa virusi hivi hatari. Tutatumia fedha za ruzuku kutoka kwa serikali kuu kuhakikisha tunaboresha miundomisingi ya shule zetu ili kufikia viwango vya uzalishaji.” Amesema.

Mkurugenzi wa idara ya vyuo vya anwai kaunti hii Raphael Chola amesema tayari wameanza mpango wa kununua vifaa vipya na vya kisasa kwa shule za kiufundi sawia na kuanzisha kozi za muda mfupi kwa lengo la kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa jamii.

Kaunti ya Taita Taveta iko na vyuo 28 vya kiufundi na wanafunzi zaidi ya 4000.

https://youtu.be/EW2RMmTHvtY

David Moto

Leave a Comment
Share
Published by
David Moto

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago