Categories: Taita Taveta News

ILANI YA KUONDOKA ARDHI YA KIKUNDI CHA MGENYI

Hapo jana wawakilishi watatu wa Bunge la Kaunti ya Taita Taveta (MCAs), walijikuta katika mkono mbaya wa serikali walipoenda kutetea wakaazi wa Kijiji cha Manga – Ngolia Wadi, wasifurushwe kwenye makaazi yao.

Hii inatokana na kuwa kikundi kimoja, ambacho hakijasajiliwa rasmi, kinadai kuwa sehemu wanakijiji hao wanakoishi, ni shamba lao.

Kikundi hicho kinachojiita, Mgenyi, kinadai umiliki wa ekari mia mbili ambamo takribani watu mia tatu wanaishi.

Cha kusikitisha ni kuwa, wana kikundi hao wakiwa na mifuko mizito na nguvu za kisiasa, wameweza kupata usaidizi wa idara ya usalama katika kaunti ya Taita Taveta kufanikisha mbinu yao ya ulaghai. Kulingana na barua yao, wanadai kuwa kumekuwa na kesi kadhaa, chini ya miti, ambazo wanakijiji walizisusia, na zote uamuzi kwa manufaa yao.

Inasemekana kuwa sehemu hiyo hiyo ndiyo serikali ya kaunti inanuiwa kujenga kiwanda cha EPZ.

Hivyo basi, wana kikundi cha mgenyi wanataka kupata umiliki wa shamba hilo ambalo linasemekana kuwa limeorodheshwa kama, Community Land, ili baadae wauzie serikali ya Kaunti ama waekezaji wa kibinafsi ili wajiundie hela zao za kibinafsi.

Wakaazi wa kijiji cha Manga wanashangaa kuona k wamba baadhi ya waliotia sahihi ya kufurushwa kwao ni viongozi wao waliowachagua kuwawakilisha katika bunge la Kaunti na la serikali kuu, kama wana kikundi gushi cha Mgenyi.

Wakaazi wanaomba serikali iingilie kati kuhakikisha hawatafurushwa na haki xao za kibinadamu zitachungwa.

Wanaomba pia kusambaziwa maji kutoka Mzima Springs ilioko karibu na kijiji hicho ili kuwaondolea tatizo la shida ya maji.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago