Categories: Taita Taveta News

GAVANA SAMBOJA AHESHIMU KINA MAMA, VIJANA WA YAM WASEMA

 

TAARIFA KUTOKA KWA UONGOZI WA YOUTH ASPIRING MOVEMENT KWA VYOMBO VYA HABARI, TAREHE 8TH MACHI, 2021 KUHUSU SHEREHE KUU YA WANAWAKE DUNIANI.

Kundi la Vijana linalotambulika kama YAM linalo furaha nyingi Leo hii wanawake wanapoisherehekea siku Yao ya Kimataifa. YAM imechukua fursa hii kutakia akina mama zetu baraka njema wanapoisherekea siku hii. Wanawake ni akina mama zetu, madada zetu, wake zetu, na zaidi ya yote viungo muhimu katika jamii yetu.

YAM vilivile inachukua fursa hii kuambia TAIFA letu tukufu kwamba itasimama na akina mama wote wale walioko uongozini na wale ambao hawako.

Fauka ya hayo, YAM imesikitishwa sana na matamshi ya Gavana Samboja kwa Muakilishi wa Akina mama Mheshimiwa Lydia Haika Mizighi kuhusiana na habari za kuchochea, na kuhonga Wahudumu wa Afya wa hii Kaunti ili wasirudi kazini.

Madai hayo hayana Msingi wowote bali Ni Uzushi tu Uliona na Nia ya Kumpaka Tope Mama Haika na pia kumkosanisha na wauguzi na pia kudhalilisha wauguzi kwamba wao ni watu wa maslahi na wasio shiba. Vilevile hii ni siasa ya uchochezi yenye Nia fiche ya kukosanisha Mama Kaunti na wagonjwa, walio na wagonjwa, na wale waliofiwa.

Governor Samboja Kama anao ushahidi Wa Kutosha wa suala hilo la Mama Kaunti kulipa wauguzi, basi angepaswa kumuita Mama Haika Wakaliongea Ajue Uhalisia wa mambo Kabla ya Kupayuka na Kuropoka Mambo Yasiyo Ya Kweli Mbele Ya Waumini Kanisani. Vilevile, angechukua hatua za kisheria kuliko kuharibia watu majina Yao Kwa minajili ya siasa. Sio vizuri Kiongozi wa haiba yake kukejeli au kukaripia Viongozi wengine na wauguzi mbele ya madhabahu ama Mbele Ya umma.

Ni hivi majuzi kwenye Hafla Ya Mchango wa akina Mama pale Kaloleni mjini Voi ukiongozwa na Senator Gedion MOI, Governor Samboja Alimkejeli Mama wa Kaunti mbele ya Hadhira akisema Mama Haika Anasakata Densi Ya Wheelbarrow Huko Matunguu. Hiyo Ilikuwa kumsuta mbele ya akina mama wenzake na kumvua nguo mbele Yao huku akiwa na nia ya kuleta picha mbaya ya Mama Kaunti kutokuwa na ushirika mzuri na mama wenzake.

Vilevile Wakili Bwire aheshimu wapiga Kura wa Taveta na akinamama na mama Mbunge wa Eneo Bunge la Taveta. Awache kumhujumu bure na semi zake zisizo na msingi kwamba Mheshimiwa Naomi Shabaan aliiba Kura ya mwaka elfu mbili na kumi na Saba (2017) na hataweza kuiba yake kwa sababu yeye ni wakili. Anachafulia mama sifa ya kuongoza Taveta Kwa miongo miwili sababu ya kutaka kugombea nafasi hiyo mwaka wa elfu mbili na ishirini na mbili (2022).

YAM imeamua kuyazungumizia maswala haya kwa sababu ya heshima ambayo wanapea jinsia ya kike (mama, dada, wake, mashemeji). Matamshi Ya Governor na Wakili Bwire ni Ya Kizushi na yakudhalilisha jinisia ya kike. Tunaomba akina mama watoke Kwa wingi ili waweze kuyazungumzia maswala haya bila uoga maana wakiendelee kunyamaza basi watawanyamazisha kabisa na masufuria, kesi kortini na matusi yaso na msingi. Viongozi wa kike wanapodhalilishwa basi kuna uwepo wa hatari Kwa wale wasio uongozini na wasio na nguvu ama sauti.

Happy international women’s Day.

YAM – Muamko Mpya Taita Taveta

Sauti Ya Wananchi – Taita Taveta

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

17 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago