Categories: Kenya Trends

BBI6: MUHTASAR I WA RIPOTI YA JOPOKAZI LA RAIS KUHUSU MAPATANO MARIDHIANO NA U MOJA WA KITAIFA

Sura ya 6 — Ushirikishwaji

Jopokazi linatoa mapendekezo makuu katika kuimarisha ushirikishwaji kwa misingi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kidini, kitamaduni, vijana, na kijinsia. Hapa kuna baadhi yake:

1. Mwandishi Maalum wa Masuala ya Ushiriki wa Umma— Kuimarisha ubora, uwazi, na ushirikishwaji katika michakato ya ushiriki wa umma unaohitajika Kikatiba kwa kubuni Ofisi ya Mwandishi Maalum wa kushughulikia Ushiriki wa Umma. Ofisi hiyo itapewa jukumu la kuandaa shughuli za kuushirikisha umma kwa niaba ya taasisi zote za serikali na zisizo za serikali zinazotekeleza mipango ya sera na utendaji ambayo, Kikatiba, inahitaji ushiriki wa umma. Mwandishi Maalum wa Masuala ya Ushiriki wa Umma anapaswa kuweka rekodi sahihi kuhusu ushiriki wa umma hadharani na aweze kukidhi haja za asasi zinazotaka huduma yake. Kando na jukumu la kuimarisha uwazi na kufanikisha ushiriki wa umma, ongezea ofisi hiyo jukumu ambalo litasababisha ubishi kuhusu maslahi ya umma kwa namna ambavyo inakingwa dhidi ya ushawishi wa msambazaji/mchuuzi. Mfano wa jinsi jambo hili linaweza kufanya kazi katika mfumo wa demokrasia unapatikana katika kielelezo cha India.

2. Jamii zilizotengwa hazifai kuwatenga wengine— Ithibati kutokana na mashauriano ya BBI katika kaunti inaonyesha maoni yenye uzito kwamba baadhi ya jamii ambazo zililalamika kuhusu kutengwa katika ngazi ya kitaifa zenyewe zilikuwa na hatia ya kutenga jamii za watu wachache katika Kaunti husika. Kwa hivyo ilikuwa wazi kuwa mageuzi ya kukuza ushirikishwaji katika ngazi ya kitaifa yanapaswa pia kuonekana katika kiwango cha Kaunti.

3. Uraia wa mataifa mawili – Kuhusu suala la Wakenya walio na uraia wa mataifa mawili kuwa wasioaminika kwa msingi huo, huo unakuwa
ubaguzi na kiwango ulinzi na utambulisho wao unarudi chini. Wakenya walio tayari kuwa watumishi wanapaswa kupimwa kwa vigezo vya tabia na utendakazi wao mzuri na si kudhaniwa kuwa wamegawa uaminifu wao kuwili, ambao unatia doa maadili na uzalendo wao. Kwa hivyo, mipaka ya uwezo wa raia wa mataifa mawili kuwahudumia Wakenya unapaswa kuwa mdogo zaidi. Mfano mmoja ni kuhusu vikosi vya ulinzi, ambavyo kikatiba vinaweza kuamrishwa kushambulia wanajeshi wa nchi nyingine ambazo vikosi hivi vinaweza kuwa na uraia nazo. Kwa kuzingatia uchunguzi huu, Jopokazi linapendekeza kwamba watumishi pekee wa Serikali wanaoweza kuwekewa mipaka ya kuwa na uraia wa mataifa mawili wawe Amiri Jeshi Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi, wanachama wa vikosi vya ulinzi, na uanachama wa Baraza la Ulinzi.

Sura ya 7 — Ustawi kwa Wote

Tunahitaji mapinduzi ya kiuchumi, ili kujenga uchumi ambao unaweza kuzalisha kazi tunazohitaji, haraka. Wakenya walioongea katika kila kikao cha mashauriano kinachoendeshwa na Jopokazi, katika kila Kaunti, walizungumzia matatizo yao yanayochangiwa na umaskini na ukosefu wa kazi au ajira za mapato duni. Changamoto moja muhimu inayokabili Wakenya kuhusu suala la ustawi wa pamoja ni kuunda kazi za kutosha na ajira, haswa kwa vijana. Haitoshi tu kuboresha uchumi wetu na kupanua uwekezaji: ni lazima tuibadilishe kabisa mfumo wa uendeshaji wa uchumi wetu ikiwa tunataka kukabiliana na ukosefu wa kazi uliopo sasa. Baadhi ya Mapendekezo machache makuu katika ripoti ni:

1. Mkakati wa miaka 50 — Tunahitaji kupanua mawazo yetu yawe ya kudumu ikiwa tunataka kujenga uchumi ambao unakidhi mahitaji ya vizazi vya sasa na vijavyo. Anza na mkakati wa miaka 50 ambao lengo lake kuu ni kuifanya Kenya iwe miongoni mwa mataifa bora zaidi ulimwenguni kwa chumi zilizostawi, za pamoja na endelevu.

2. Kujenga masoko kana kwamba ni bidhaa za umma — Serikali inapaswa kuwa katika harakati za kuendelea kujenga masoko na kuyapanua masoko hayo kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa na nguvu kazi ya Wakenya katika mataifa jirani kupitia utangamano zaidi.

3. Kutoa mikopo kwa sekta muhimu — Serikali inapaswa kubuni sera inayotoa miongozo ya kisheria na kiudhibiti kwa benki ili ziweze kutoa mikopo kwa sekta muhimu kama za biashara ndogo ndogo, uuzaji bidhaa nje ya nchi, uzalishaji, makazi, elimu, afya, nishati mbadala, usafi wa mazingira na utupaji wa taka, na kilimo (ikiwemo mifugo na uvuvi).

4. Ustawi wa viwanda unahitaji kuwa lengo kuu la Serikali – Ni ustawi wa viwanda pekee unaoweza kukuza vipaji vya Wakenya na ni ndoto ya kuendeleza ustawi wa taifa. Ni muhimu kwa Wakenya na Serikali kujitenga na gumzo linaloshamiri kwamba Kenya na mataifa ya Afrika hayawezi kujistawisha kiviwanda kwa sababu ya kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia, kwa mfano katika matumizi ya roboti.

5. Kulinda uvumbuzi wa Wakenya, rasilimali za kinasaba, maarifa ya jadi na misemo kama aina ya mali iliyolindwa kisheria – Mustakabali wa uchumi wa dunia uko katika ubunaji na uvumbuzi kwa kutumia utaalamu wa kiakili, uundaji ramani na matumizi ya msimbo wa kinasaba, na hazina hai ya maarifa ambayo imeandaliwa na vizazi vya jamii zetu.

6. Akiba ni uwekezaji — Fanya juhudi kubwa ya kuongeza akiba ya kitaifa kwa angalau asilimia 25 ya Pato la Taifa ikiwa Kenya inataka kuendeleza uwezo wake wa kuimarisha uwekezaji katika sekta mbalimbali, kikiwemo kituo cha nguvu kazi madhubuti cha uzalishaji ili kuunda nafasi za kutosha za kazi kwa Wakenya
7. Mapato kutoka kwa Wakenya waishio ng’ambo– Usitegemee pesa kutoka ng’ambo pekee bali toa vivutio, kinga na taratibu za kuruhusu Wakenya wanaoishi ng’ambo kuweka zaidi akiba zao nchini Kenya.

8. Tumia pesa kwa maendeleo, si kwa urasimu pekee – Tumia pesa nyingi kwenye maendeleo kama sehemu ya mapato ya serikali ili kuongeza bidhaa za umma na huduma kwa Wakenya. Lenga uwiano au kikomo cha juu, ulioandikwa kuwa sheria, wa angalau 70:30 kwa maendeleo dhidi ya matumizi ya kawaida.
9. SRC na mishahara— Ni sharti kuwe na ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kisheria na kiutawala ya Tume ya Mishahara na Marupurupu ili kuhakikisha kuwa inasimamia masuala yote yanayohusiana na nyongeza za mishahara.

10. Ushuru — Ijapokuwa mawanda ya ushuru yanahitaji kupanuliwa ni muhimu kwamba utozaji wa jumla wa ushuru nchini Kenya uwe chini kiasi kwa chumi shindani za kieneo na kimataifa. Wazia mbinu mpya za kurahisisha utozaji ushuru, ikiwemo fikra ya kuanzisha kiwango Sawa cha Ushuru kwa mapato ya juu kuliko ya Mshahara Unaokidhi Mahitaji ya Kimsingi.

11. Lenga wakulima, wafugaji na wavuvi — Lipe kipaumbele suala la kumaliza ufisadi miongoni mwa wanaotekeleza miradi ya kilimo na

ufugaji katika juhudi za kupambana na uovu huo. Imarisha viwanda vya mashambani kama msingi wa kuendeleza aina za kisasa zaidi za uzalishaji.
12. Kuimarisha Kifungu 43 cha Katiba kuhusu haki za kiuchumi na kijamii
i.
i. SerikaliSerikali yaya KitaifaKitaifa nana SerikaliSerikali zaza KauntiKaunti zinapaswazinapaswa kubunikubuni serasera nana kakanuninuni zaza kuongozakuongoza utekelezwajiutekelezwaji kwakwa uangalifuuangalifu wawa KifunguKifungu chacha 4343 chacha HakiHaki zaza KiuchumiKiuchumi nana KijKijamiiamii..
ii.
ii. ManifestoManifesto zaza vyamavyama —- KifunguKifungu 4343 chacha HakiHaki zaza KiuchumiKiuchumi nana KijamiiKijamii kinapaswakinapaswa kutekelezwakutekelezwa kwakwa uangalifuuangalifu nana viongoziviongozi wotewote waliochaguliwawaliochaguliwa nnaa manifestomanifesto zotezote zaza uchaguziuchaguzi zaza vyamavyama vyaovyao vyavya kikisiasa.siasa. HiiHii itahitajiitahitaji VyamaVyama vyotevyote vyavya SiasaSiasa kuundakuunda maonomaono nana serasera zaza utekelezwajiutekelezwaji wawa MswadaMswada wawa HakiHaki (unaojumuisha(unaojumuisha HakiHaki zaza KiuchumiKiuchumi nana Kijamii)Kijamii) kamakama sehemusehemu yaya manifestomanifesto zaozao zaza kampenikampeni zaza uchaguziuchaguzi.

13. Hakuna Mkenya ataachwa nje —’Mpango wa Kubadili’: Kama sehemu ya kuhakikisha kwamba Wakenya wote wanapata huduma bora ambazo ndio msingi wa kuwaweka watu kwenye njia ya ustawi wa pamoja, Jopokazi linapendekeza ‘Mpango wa Kubadili’ ili kuyavuta maeneo yaliyotengwa hadi kwenye kiwango bora kinachostahiwa maeneo mengine.

14. Tumia rasilimali chache za umma kwa maendeleo, si kwa urasimu pekee — Tumia pesa nyingi kwa maendeleo kama sehemu ya mapato ya serikali ili kuongeza bidhaa za umma na huduma kwa Wakenya. Lenga uwiano au kikomo cha juu, ulioandikwa kuwa sheria, wa angalau 70:30 kwa maendeleo dhidi ya matumizi ya kawaida.

15. Kuza na fungua nafasi kwa vijana ili waonyeshe mipango, ubunifu na ujasiriamali wao— Kwa kuongeza nafasi za ajira na njia za kupata riziki kwa kufanya biashara ndogo ndogo zishindane kwa urahisi na kukua bila Serikali kuziwekea mazingira magumu na ghali kwao kufanya kazi.

i. Taifa liandae na kuzindua mbinu rahisi za wanabiashara wadogowadogo wa Kenya kufanya biashara na kutotegemea vielelezo vya kuf anya biashara vinavyoandaliwa na wageni kwa ulinganishi wa kimataifa. Hii inapaswa kuwa tathmini linganishi ya
KNBS ya kila mwaka ambayo haijagawanywa kijiografia kaunti, majiji na miji na itangazwe

ii. Punguza kutoza biashara ndogondogo na mpya ushuru kwa kuwapunguzia ushuru kwa angalau miaka saba kama njia ya kuinua ujasiriamali wa vijana na uundaji wa nafasi za kazi

iii. Ubunifu na michezo Fanya juhudi za kimakusudi za kuratibu, kuhamasisha na kukuza ubunifu na michezo, miongoni mwa sekta nyingine ambazo vijana wa Kenya huonyesha uwezo mkubwa na ari.

iv. Himiza Sekta ya Kibinafsi kuunda wakfu wa kitaifa, usio wa biashara ambao utasimamiwa na Rais na ambao utatumiwa kutoa ushauri, mafunzo, na zana za kuwasaidia vijana wa miaka 18 35 wanaopania kuwa wafan yabiashara.

v. Ili kuwasaidia vijana kuanzisha biashara, fungua meza ya ushauri katika kila Kituo cha Huduma Centre kinachosimamiwa na mtaalamu wa maendeleo ya kibiashara

vi. Kujiajiri na Elimu ya kiufundi Ni muhimu tuondoe dhana kwamba kazi ya ufundi ni ya wa le ambao wameshindwa katika masomo kwa kuunda njia mbili sawa kati ya mafunzo ya kitaaluma na ya ufundi.

Sura Ya 8 — Ufisadi

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

5 hours ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

8 hours ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

1 day ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

2 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

4 days ago

TAITA TAVETA: WE CANNOT CONTINUE THIS WAY — A COUNTY GOVERNMENT IN CRISIS OF ACCOUNTABILITY

Kwaela News Network | Editorial Taita Taveta County is confronting a governance crisis that can…

6 days ago