Categories: Kenya Trends

BBI10: MUHTASAR I WA RIPOTI YA JOPOKAZI LA RAIS KUHUSU MAPATANO MARIDHIANO NA U MOJA WA KITAIFA

Sura ya 10 — Usalama na Ulinzi

Wakenya waliambia Wanajopo kwamba hawajisikii salama. Jopokazi lilibaini kwamba Kenya iko katika eneo hatari na vitisho vya ugaidi vinavyozidi kujitokeza, mataifa yenye utawala unaoyumba au dhaifu na nchi zenye mizozo ya kimipaka, unyanyasaji wa polisi na matendo haramu ya kijambazi yanayokiuka haki za binadamu. Jopokazi linapendekeza hatua madhubuti zifuatazo:

1. Sawazisha thamani ya maisha ya Mkenya katika kila sehemu ya nchi -Thamani ya maisha iliyoathiriwa na vurugu, ukosefu wa usalama na viwango duni vya usalama inapaswa kuwa sawa kote Kenya. Ni sharti tuache mazoea ya dhana kwamba kuna matokeo tofauti ya vurugu katika sehemu tofauti ya nchi. Kufanya mabadiliko haya kunahitaji usawa katika usambazaji wa maafisa wa polisi, mashtaka na juhudi za kuzuia uhalifu.

2. Mkakati wa Usalama wa Kitaifa unaojivuniwa na raia — Baada ya kugundua kuwa usalama ni wa raia, tunahitaji mbinu inayozingatia usalama wa kibinadamu iwekwe katika Mkakati kamili wa Kitaifa wa Usalama na Ulinzi (kila baada ya miaka miwili na kila Rais anayeingia mamlakani katika kipindi cha miezi mitatu baada ya kuchukua hatamu za uongozi) na ambayo inamilikiwa na watu na serikali yote. Inapaswa kuwa amilifu, yenye kuzuia, na ya kutahadharisha.

3. Kutoathiriwa sana na migogoro ya rasilimali, majanga, dharura na uhaba wa chakula kwa kutekeleza Mkakati kamili wa Dharura za Kitaifa, Mkakati wa Kushughulikia Maafa na Migogoro uliowekwa kwenye sheria ambayo inahusishwa na mipango ya kukabiliana na majanga katika ngazi ya kaunti, kaunti ndogo na wadi ambayo husasishwa mara kwa mara.

4. Ugaidi ni tishio linaloendelea kuathiri Wakenya ambao wanahitaji zana mbalimbali kulishughulikia, si usalama tu – Kukabiliana na Ugaidi kutafanikiwa tu ikiwa utahusishwa zaidi na ulinzi wa kisiasa, kijamii na kitamaduni ambao hupunguza idadi ya wanaosajiliwa, na kutohalalisha malengo ya maadui wetu.

i. Kuangazia na kuratibisha mipango ya kuzuia itikadi kali na mafunzo yanayochochea vurugu katika Wizara zinazohusika na afya, elimu, vijana, utamaduni na turathi.

ii. Kuhusu namna Fedha za Kulinda Waathiriwa zinavyotumiwa, waathiriwa wa ugaidi wanapaswa kupewa kipaumbele kwa kuwa kunyanyaswa kwao kunalenga kutishia Wakenya wote moja kwa moja pamoja na viongozi tuliochagua kwa misingi ya kisiasa, kijamii na kidini.

5. Masuala ya Kigeni— Kutathmini mahusiano ya kidiplomasia na mataifa yanayofadhili ugaidi, misimamo mikali ya kidini, na upanuzi au kujitenga Hakikisha diplomasia imeundwa na kufadhiliwa ili kukabiliana na vitisho vinavyoibuka kabla ya kudai mwitiko madhubuti wa usalama. Kuhusiana na bajeti, ni muhimu kwamba Wizara ya Masuala ya nje, inapata mgao sawa na Idara ya Ulinzi, Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS), na vyombo vingine vya usalama.

6. Utendakazi wa polisi, na afya ya akili na ustawi – Kuimarisha utendakazi na huduma za Shirika la Huduma za Kitaifa za Polisi, pamoja na kuboresha afya ya akili na ustawi wa maafisa hao.

i. Fafanua Viashiria Muhimu vya Utendakazi kwa makamanda wa polisi kutoka katika ngazi ya Inspekta Jenerali wa Polisi hadi chini kwa kitengo cha umma cha kuripoti takwimu za uhalifu wa kitaifa na ukosefu wa usalama. Vitengo hivi viwili vizingatiwe katika kupandisha vyeo na kutoa vivutio.

ii. Unga mkono maadili na utendakazi bora katika NPS kwa kutambua na kutuza ufanisi, kujituma na kujitolea kwa maafisa na wananchi.

iii. Kama suala la kipaumbele, pawe na huduma za ushauri kuhusu afya na matibabu ya akili ya maafisa wa polisi. Polisi walio na majukumu makubwa ambayo yanawaweka katika hatari ya kudhurika kiakili wapewe mazingatio maalum. Hatua zote zinapaswa pia kuchukuliwa ili kuweka familia pamoja.

7. Linda Wananchi dhidi ya vitisho vya kibinafsi na hatari

i. Kukabiliana na visa vya unyanyasaji wa kijinsia na ngono kupewe kipaumbele kwa kuzingatia na kutoa rasilimali maalum kwa polisi na kuchukua hatua za kuzuia dhuluma za kijinsia na ngono.

ii. Shughulikia mizozo ya mipaka ambayo inahatarisha usalama wa kitaifa na jamii – Unda tume maalum au majopokazi kwa kila mzozo wa mpaka ili washauriane na wadau wote na kutoa mapendekezo ya mageuzi ambayo yatashughulikiwa.

iii. Wafichuzi wa uhalifu walindwe — Wezesha taratibu za mahakama ambazo zitahakikisha usalama na ulinzi wa watoaji habari, wafichuzi na mashahidi, hususan wa ugaidi, uhalifu mkubwa wa kimataifa, na ufisadi.

iv. Utatuzi wa migogoro inayokumba wananchi – Imarisha ujuzi wa raia wa kutatua migogoro na upatanishi katika mfumo mzima wa elimu ya Kenya. Fanikisha hili kwa kujumuisha maarifa ya utatuzi wa migogoro, mazungumzo na ushauri katika mtaala wa elimu katika ngazi zote za elimu ya msingi na sekondari.

v. Linda Wakenya dhidi ya vyakula hatari kwa kuimarisha usimamizi wa usalama wa chakula.

Sura ya 11 — Tume na Masuala Yanayogusa kila kipengee

1. Tenganisha kazi ya kuchunguza makosa ya uhalifu na ile ya kupandisha vyeo na kuhakikisha maadili yamezingatiwa katika utumishi wa umma. Kazi ya kuripoti kuhusu kupandisha vyeo na utekelezaji wa maadili itafanywa na Tume iliyopendekezwa ya Maadili inayozungumziwa katika sura ya maadili ya kitaifa.

2. Bainisha majukumu ya mashirika ya udhibiti ili kuhakikisha kwamba hakuna urudiaji wayo, na kurahisisha uwazi, pawe na huduma za haraka zinazopatikana gharama nafuu ili sheria ya udhibiti ifuatwe kwa viwango vya juu.

3. Kuimarisha Maabara ya Serikali ili kuifanya iwe imara katika utekelezaji wa majukumu yake.

4. Unda taasisi madhubuti iliyoungana ya kudhibiti na kuhakikisha usalama wa chakula.

5. Kaunti ya Nairobi – Ni kaunti tofauti na nyingine kutokana na ukweli kwamba ndio mji mkuu wa taifa ulio na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN). Ofisi za UN jijini Nairobi ni makao makuu ya tatu ya Umoja huo ulimwenguni. Ndio sababu ni tofauti na kaunti nyingine. Wakenya wanaustahi mji huu mkuu kuwa wenye vitengo vyote vikuu vya Serikali na kama eneo muhimu kwa ushiriki wao wa mijadala ya uraia katika maisha ya kitaifa. Hii ina maana kuwa Tume ya Ugavi wa Mapato inaweza kujitahidi kuzingatia hadhi hii maalumu ya Nairobi na mahitaji ya huduma ambayo huja nayo.
Zaidi ya kuuzingatia kama mji mkuu, makubaliano ya tarehe 26 Machi 1975 kati ya Jamhuri ya Kenya na Umoja wa Mataifa kuhusiana na makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira jijini Nairobi yanabainisha hatua za Serikali ya Kitaifa kuboresha mazingira, miundo msingi, huduma za umma, na ufikiwaji wa makao makuu haya. Hatua hizi zinakubaliwa na Serikali ya Kitaifa na si Serikali ya Kaunti. Hadhi ya Nairobi kama mwenyeji wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ni sababu kubwa ya kuwa kitovu cha kidiplomasia ambapo nchi kadhaa huanzisha ujumbe maalum ambao huruhusu uwakilishi katika UNEP na mashirika mengine ya UN yanayoendeshwa kutoka Nairobi. Jopokazi linapendekeza kwamba Nairobi ipewe hadhi maalum ya mji mkuu ambao unaipa Serikali ya Kitaifa njia ya kutoa huduma na uwezeshaji ufaao katika kuudumisha kama mji mkuu na kama kitovu cha kidiplomasia. Kwa wakati huo huo, hadhi maalum kama hiyo haifai kuzuia haki za wakazi wa Nairobi za uwakilishwaji katika ngazi za wadi na bunge.

6. Kuteua Makamishna wa IEBC — Mkutano wa Viongozi wa Vyama Kisiasa Bungeni utateua kwa makubaliano, watu watakaopendekezwa kuteuliwa na Rais kama makamishna wa IEBC. Wanaosaka nafasi hiyo wanapaswa kufikia vigezo vilivyoainishwa katika Katiba na sheria na hawapaswi kuegemea upande wowote, na rekodi ya uadilifu na mambo walioyaafiki, na ambao si wanachama maarufu wa chama cha kisiasa na hawana rekodi ya kuchukua nafasi za umma kwa msaada ya chama.

7. Makamishna wa muda — Nusu ya Makamishna katika Sura ya 15 kuhusu Tume, isipokuwa kwa IEBC, wanapaswa kuhudumu kwa muda maalum.

8. Ni sharti kila tume huru iwe na mifumo ya ndani ya uwajibikaji ambayo hutenganisha kwa njia huru na wazi mamlaka ya uteuzi na kupandisha vyeo na yale ya kusimamisha kazi na kusuta.

9. Ukaguzi mkali wa mahesabu unaochunguza thamani ya matumizi ya pesa na kuendeleza kanuni bora za usimamizi wa fedha za umma unapaswa kutumika katika kila kitengo cha serikali na kila asasi ya umma.

10. Kifungu cha 249 (3) kimekiukwa na hii imeathiri uwezo wa Tume za Sura ya 15 na ofisi huru kutekeleza ipasavyo na kwa njia huru majukumu yao. Wakati huo huo, Tume na ofisi huru pia zinapaswa kupitia ukaguzi mkali na mashirika yafaayo ili kuhakikisha kuwa zinatimiza majukumu yao kama inavyotakiwa.

11. Jumuisha mabaraza ya usimamizi – Hivi sasa, karibu kila sheria huanzisha mamlaka fulani ya udhibiti au nyingine pia hubuni baraza fulani la rufaa kusuluhisha mambo yanayotokana na zoezi la wadhibiti wa mamlaka yake ya kisheria. Uhusiano kati ya mdhibiti na mabaraza haya umekosesha maana mantiki ya hukumu zisizoegemea upande wowote katika kuamua mizozo. Isitoshe, idadi kubwa ya mabaraza ya hukumu yaliyobuniwa kwa njia huishia kufuja rasilimali za kitaifa pakubwa. Inapendekezwa kuunda Baraza Moja la Rufaa ya Kitaifa ambalo litasikiza na kuamua kesi tofauti za rufaa (kama vile, nguvu na kawi, michezo, na mazingira).

12. Punguza idadi ya mashirika ya udhibiti kwa kufanya juhudi kubwa za kurahisisha uoanishaji na majukumu yao. Lengo ni kuwa na kanuni chache na zenye kutekelezwa kwa njia bora, na zawadi dhidi ya rushwa katika mchakato huu.

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

18 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

6 days ago