Categories: Business

ATHANAS MBELE AWASILISHA PETISHENI BUNGENI DHIDI YA KAMPUNI ZA MIKOPO ZINAZOWANYANYASA WAKAZI WA TAITA TAVETA

 

Taita Taveta, Kenya — Kiongozi wa jamii na mwanaharakati Athanas Mbele ame wasilisha petisheni kwa Bunge akitaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya kampuni za mikopo zinazodaiwa kuwahangaisha wakazi wa Kaunti ya Taita Taveta.

Kupitia taarifa yake, Mbele alizishutumu kampuni kadhaa za mikopo, zikiwemo Sherlock na zingine, kwa kujihusisha na utoaji wa mikopo ya riba haramu (usury) bila vibali kutoka Benki Kuu ya Kenya (CBK).

“Kampuni za mikopo lazima ziacha tabia ya kuwahangaisha wakazi wa Taita Taveta, kama ilivyo kwa Sherlock na zingine. Bila barua za kibali kutoka Benki Kuu ya Kenya (CBK), shughuli zao ni riba haramu (usury) ambayo imepigwa marufuku kisheria nchini Kenya,” alisema Mbele.

Aliongeza kuwa kampuni hizo hazinyanyasi tu wananchi bali pia zinawakandamiza wafanyakazi wao, hazilipi kodi, wala kutimiza wajibu wao wa kisheria. Kulingana naye, kampuni hizo zimefukuzwa katika kaunti nyingine na sasa zimehamia Taita Taveta zikiwa na lengo la “kudhoofisha uchumi wa wenyeji kwa kisingizio cha ukusanyaji wa madeni.”

Mbele alisisitiza umuhimu wa kusajili na kudhibiti ipasavyo kampuni zote za mikopo zinazofanya kazi katika kaunti hiyo. Pia alitoa wito kwa kampuni hizo kuwa na uwazi katika utoaji mikopo, kuweka sera za haki za ulipaji, na kushiriki katika miradi ya kijamii (CSR) inayowanufaisha wananchi wa eneo hilo.

“Tunazitaka kampuni hizi zisajiliwe ipasavyo, ziendeshe shughuli kwa uwazi, na zitoe mikopo kwa uwajibikaji,” alisema Mbele. “Huwezi kuendelea kukopesha watu hadi wanaugua na kuwa maskini halafu udai unaleta maendeleo.”

Aidha, Mbele alipendekeza kampuni hizo kufungua ofisi zao kuu ndani ya Kaunti ya Taita Taveta ili kudhibiti mtiririko wa mitaji nje ya eneo hilo na kuhakikisha uwajibikaji wa ndani.

Petisheni hiyo sasa inasubiri kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Fedha na Mipango ya Kitaifa, ambayo itaamua iwapo itazialika kampuni husika pamoja na wadhibiti wa sekta kwa uchunguzi zaidi.

Iwapo petisheni hiyo itapitishwa, inaweza kuweka msingi mpya wa kudhibiti zaidi kampuni za mikopo zinazotumia mbinu za unyonyaji katika kaunti mbalimbali nchini Kenya.

Gusa hapa kuta PETISHENI sahihi!

Kwaela News Network

Leave a Comment
Share
Published by
Kwaela News Network

Recent Posts

TAITA TAVETA: SEVEN DAYS HAVE ELAPSED — HAS SENATOR KAJWANG SENT WAKUJAA’S GOVERNMENT FILES TO EACC?

  By Kwaela News Network (KNN) | Governance & Accountability The seven-day ultimatum issued to…

16 hours ago

THE ERA OF POLITICAL EUPHORIA IN TAITA TAVETA COUNTY IS OVER

  The days when political party waves and symbolism single-handedly determined election outcomes in Taita-Taveta…

1 day ago

TAITA TAVETA: CAN THE DCI CRACK THE NUT? DORCAS MLGHU’S PUBLIC OUTBURST PUTS COUNTY EXECUTIVE UNDER FRESH PRESSURE

  The growing controversy surrounding the financial management of Taita Taveta County has taken another…

2 days ago

THE GOVERNOR DISCOVERS FISCAL DISCIPLINE — FOUR YEARS TOO LATE?

  Perhaps one of the most ironic moments of Governor Andrew Mwadime's appearance before the…

3 days ago

NDARA B LAND DISPUTE: 63 RESIDENTS SERVED WITH THREE-MONTH EVICTION NOTICE FOLLOWING COURT RULING

Affected families in Mlambenyi, Golani and Mto Mwagodi face a February 2027 deadline as the…

3 days ago

THE WRONG TIME: GOVERNOR WAKUJAA’S DEFENCE

During a Senate Public Finance Committee meeting, Taita Taveta Governor Andrew Mwadime, popularly known as…

5 days ago